Monday, March 4, 2013

Mashabiki wa Man Utd wakesha Airport kumsubiri Ronaldo

Mashabiki wa mpira wamejitokeza kwa wingi Airport jijini Manchester kumpokea mchezaji wa kimataifa anayekiputa Real Madrid"miamba ya Hispania"
Mashabiki hao waliokesha Airport ucku kucha walifanikiwa kumuona CR7 akiongozana na Bosi wake Jose Mourinho
Real Madrid imeingia jijini Manchester kukamilisha mchezo wao dhidi ya Manchester United utakaopigwa siku ya Jumanne Katika dimba la Old Trafford ikiwa Ni mara ya kwanza Kwa mchezaji huyo kutua Manchester tangu auzwe kwenda Real Madrid kwa Ada ya £80 millioni
Miamba hiyo ya Hispania wamepewa uwanja wa kufanyia mazoezi na Manchester city ili kupambana na maadui zao siku ya Jumanne tarehe 5 saa 3:45 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki ikiwa Ni mchezo wa marudiano ambapo walitoka sare ya moja kwa moja

Habari na;JACOB JOSEPH















Foleni ya Maloli yasababisha Vurugu kurasini

Foleni Kubwa iliyosababishwa na Maloli ya kampuni ya mafuta ya Puma (zamani BP) yakiwa yamepanga foleni kuingia ndani ya ofisi zao zilizopo Keko ambapo ndio makao makuu.

Foleni hiyo iliyoanza tangu saa tano asubui hadi sasa bado inasemekana haijapatiwa ufumbuzi imesababisha watu kutembea kwa umbali mrefu

Tafadhali wahusika wazingatie shughuli nyingi za ujenzi wa Taifa zinakwama

Habari na;JACOB JOSEPH









Sunday, March 3, 2013

Daladala lapinduka Magomeni mikumi lajeruhi

Daladala linalofanya safari zake hapa Dsm Buguruni na kawe limeacha njia na kupinduka maeneo ya Magomeni mikumi majira ya saa Saba mchana.

Hata hivyo hakuna taarifa za mtu aliyepoteza maisha mpaka tunarusha Habari hii,

Habari na;JACOB MBUYA









Saturday, May 5, 2012

BIG BROTHER TZ WEMA AU JOKATE?

WALE WALIMBWENDE wawili wakibongo ambao kila kila m2 ukimuuliza kuwa anamjua WEMA o JOKATE hakika basi hata mtoto mdogo atakwambia yule mchumba wake diamond?

Hicho ndo kitu kilichowaweka hawa wadada juu kuliko anythng hapa bongo achilia mbali walishiliki Vodacom miss Tanzania mwaka 2006 na mmoja akawa wa kwanza na mwingine akafatia.

Mimi hadi leo ukiniuliza nani mzuri ntakosa jibu la kukupa zaidi ntakuuliza na wewe nani alikuwa wa kwanza kwenye miss TZ 2006,

Sasa hapa wameingia tena kwenye mashindano ya kumjua nani ataiwakilisha TZ kwenye jumba hilo la BIG BROTHER AFRICA na mzigo wa mwaka huu ni zaidi ya millioni 500 fedha za madafu wakati kila mmoja akiongea lake mara jokate wengine wema achilia mbali wamo mastaa kibao kwenye kinyang'anyiro hicho lakini hao ndo walopewa kipau mbele mpaka sasa sasa washiriki washafika 12 4 moo details chek




Friday, May 4, 2012

PREZOO ndani ya BIG BROTHER AFRICA STARGAME



Msanni mahiri wa nchini Kenya Jackson anayejulikana kwa jina la PREZOO leo hii ametangazwa rasmi kwenda big brother kuiwakilisha nchi yake kinyang'anyiro hicho kilicho ibua hisia za Masupa dupa weengi karibu kila nchi kinaonekana kuanza hivi karibuni.

Tanzania hii bado kitandawili kwa hakika hakuna hata mmoja anayefahamu nani kachaguliwa imeonekana nchi nyingi wasanii na mastaa wengi hutaka kwenda kwenye jumba hilo kwa kutaka kuongeza ustaa wao lakini siyo kufata mzigo(hela)mpaka sasa washachaguliwa washiriki 7.

Dkb kutoka ghana,Lady may wa Namibia,Goldie Nigeria,Barbz SA,Mampi Zambia,na Roki wa Zimbabwe mpaka sasa kitendawili kimebaki kwa waTanzania kuwa nani ataenda mwaka huu mimi wewe wote hatujui tusubiri tuone.

  Kumbuka mwaka huu mzigo ulowekwa mezani ni dola 300,000 za kimarekani kwa hela ya madafu ni zaidi ya millioni 500


Tuesday, May 1, 2012

MTOTO WA AJABU HUYU HAPA

MTOTO mwenye maumbile ya ajabu akiwa na jinsia mbili za kiume na moja ya kike amezaliwa Aprili 25 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea. Mtoto huyo ambaye bado yupo hai chini ya uangalizi maalum amezaliwa akiwa na hitilafu katika maumbile yake ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na nusu ya ubongo ambayo imetokana na hitilafu kwenye mfumo wa kichwa hadi uti wa mgongo.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa ambako mtoto huyo anaangaliwa Agness Mwinuka amesema mtoto huyo ambaye amezaliwa na uzito wa kilo moja na gramu 900 amezaliwa akiwa na jinsia mbili za kiume na jinsia moja ya kike. “Jinsia moja ya kiume ipo kama kawaida isipokuwa jinsia moja ya kiume ipo kichwani karibu na kisogo na jinsia ya kike ipo utosini,mtoto huyu tangu azaliwe juzi hadi sasa hana uwezo wa kunyonya wala kula kitu chochote ,uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea’’,alisisitiza. 

Mama mzazi wa mtoto huyo Situmahi Mwinuka(32) mkazi wa Msamala mjini Songea anasema huyu ni mtoto wake wa nne kuzaliwa na kwamba watoto wake wengine watatu hawajawahi kupata hitilafu yeyote katika mwili. Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dk.Mathayo Chanangula akielezea hali ya mtoto huyo alisema mtoto anakabiliwa na tatizo ambalo kitaalam ni hitilafu kwenye mfumo unaoanzia kichwani hadi kwenye uti wa mgongo ambao umesababisha mtoto huyo kuzaliwa na nusu ya ubongo. Kulingana na daktari huyo hitilafu hiyo imesababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari ambapo kuna sehemu mbili za kiume moja ikiwa kichwani na kwamba mtoto anapolia sehemu ya kiume ya kichwani inasimama na kusisitiza kuwa maisha ya mtoto huyo ni mafupi kutokana na mifumo ya mwili wake kutokamilika licha ya kwamba mtoto amezaliwa na miezi tisa.

 “Katika nchi zilizoendelea madaktari bingwa na wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha ya mtoto huyo,hata kama mtoto huyo anaokolewa atakabiliwa na tatizo kubwa la ulemavu wa akiri kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa binadamu kamili’’,alisisitiza. Dk.Chanangula anabainisha kuwa mama mjamzito anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo atakosa madini aina ya folic acid ambayo alisisitiza ni muhimu kwa mama mjamzito kunywa madini hayo miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake. “Mama anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya mwanzo katika ujauzito wake atatumia dawa aina ya flagile,dawa za minyoo,tetesakline na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo anaruhisiwa kunywa baada ya wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa kutumika kwa mjamzito kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa bila kumuona daktari’’,alisisitiza. Katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma hili ni tukio la kwanza la aina yake mtoto kuzaliwa akiwa na hitilafu kubwa katika mifumo ya mwili wake.

SOURCE:JamiiForum