MTOTO mwenye maumbile ya ajabu akiwa na jinsia mbili za kiume na moja
ya kike amezaliwa Aprili 25 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika
hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea. Mtoto huyo ambaye bado yupo
hai chini ya uangalizi maalum amezaliwa akiwa na hitilafu katika
maumbile yake ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na nusu ya ubongo ambayo
imetokana na hitilafu kwenye mfumo wa kichwa hadi uti wa mgongo.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa ambako
mtoto huyo anaangaliwa Agness Mwinuka amesema mtoto huyo ambaye
amezaliwa na uzito wa kilo moja na gramu 900 amezaliwa akiwa na jinsia
mbili za kiume na jinsia moja ya kike. “Jinsia moja ya kiume ipo kama
kawaida isipokuwa jinsia moja ya kiume ipo kichwani karibu na kisogo na
jinsia ya kike ipo utosini,mtoto huyu tangu azaliwe juzi hadi sasa hana
uwezo wa kunyonya wala kula kitu chochote ,uchunguzi wa kitabibu bado
unaendelea’’,alisisitiza.
Mama mzazi wa mtoto huyo Situmahi Mwinuka(32)
mkazi wa Msamala mjini Songea anasema huyu ni mtoto wake wa nne kuzaliwa
na kwamba watoto wake wengine watatu hawajawahi kupata hitilafu yeyote
katika mwili. Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma
Dk.Mathayo Chanangula akielezea hali ya mtoto huyo alisema mtoto
anakabiliwa na tatizo ambalo kitaalam ni hitilafu kwenye mfumo unaoanzia
kichwani hadi kwenye uti wa mgongo ambao umesababisha mtoto huyo
kuzaliwa na nusu ya ubongo. Kulingana na daktari huyo hitilafu hiyo
imesababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari ambapo kuna sehemu mbili za
kiume moja ikiwa kichwani na kwamba mtoto anapolia sehemu ya kiume ya
kichwani inasimama na kusisitiza kuwa maisha ya mtoto huyo ni mafupi
kutokana na mifumo ya mwili wake kutokamilika licha ya kwamba mtoto
amezaliwa na miezi tisa.
“Katika nchi zilizoendelea madaktari bingwa na
wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha ya mtoto huyo,hata kama
mtoto huyo anaokolewa atakabiliwa na tatizo kubwa la ulemavu wa akiri
kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa binadamu
kamili’’,alisisitiza. Dk.Chanangula anabainisha kuwa mama mjamzito
anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo atakosa madini
aina ya folic acid ambayo alisisitiza ni muhimu kwa mama mjamzito kunywa
madini hayo miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake. “Mama anaweza
kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya
mwanzo katika ujauzito wake atatumia dawa aina ya flagile,dawa za
minyoo,tetesakline na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo
anaruhisiwa kunywa baada ya wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa
kutumika kwa mjamzito kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa
bila kumuona daktari’’,alisisitiza. Katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma
hili ni tukio la kwanza la aina yake mtoto kuzaliwa akiwa na hitilafu
kubwa katika mifumo ya mwili wake.
SOURCE:JamiiForum