Friday, April 13, 2012

Asota jela kisa Kanumba

picha na freebongo
POLISI mkoani Pwani inatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote mkazi wa Misugusugu wilayani Kibaha Mariam Elias (19) akituhumiwa kutaka kujiua kwa kukusudia.

Mariam inadaiwa alitaka kujiua kwa kunywa sumu ya panya kwa kile alichokielezea mwenyewe kuwa ni masikitikio yake kutokana na kifo cha msanii maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa juzi jijini Dar es Salaam Jumanne.

Akizungumza na blog hii jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema taarifa za binti huyo kutaka kujiua wamezipata na kwa kuwa bado yupo hospitalini Tumbi akiendelea na matibabu amewekwa chini ya ulinzi mpaka hali itapokuwa nzuli watampeleka mahakamani.

No comments:

Post a Comment