Jina halisi anaitwa Raymond Mshana akiwa na umri wa miaka 25 tuu.
Raymond amesoma shule ya msingi Olimpio na kufaulu darasa la saba na kuchaguliwa kwenda shule ya Azania hata hivyo wazazi wake walikataa na kuamua kumpeleka mkoa wa Kilimanjaro katika shule ya Marangu secondary huku ndipo alipo gundua ana kipaji cha kuimba ambapo kila concert ya shule lazima apande kuimba watu walimjua kupitia uwezo wake wa ku rap kama Twista(Tong twist)na kupata mashabiki wengi mpaka anamaliza form 4.
Ray alirudi Dsm kuanza form 5 katika shule ya Mbezi beach high school na kumaliza akiwa na akili ya kujiendeleza ki music coz waTanzania tunajua kua mtoto lazima asome ili awe na maisha mazuri baadae hata kama ana kipaji gani mzazi hajali hilo.
So jamaa alipomaliza fom6 alipata zali la kufanya kazi NMB kwa muda usiopungua miez7 hadi alipojiunga na chuo cha usimamizi wa fedha IFM,alipofika pale sasa ikabidi aanze kusoma kweli ila akaona matangazo kila sehemu ya C2C kuwa kama unaweza utangazaji uwende kwenye usaili Ray hakusita alienda ila alipofika huko alikuta bonge la kundi la watu kwenye usaili na ikabidi jamaa akomae mpaka kuchaguliwa mmoja wapo kati ya watu wanne,Zamaradi mketema,Mussa George(kipanya),Abuubakar na Raymond Mshana.
Hapo ndio maisha yake ya utangazaji yalipoanza kwa kuanza na kipindi cha Zege alichokuwa akitangaza na kuhariri hapohapo C2C lakini maisha yaliendelea kuwa magumu siku hadi siku pale alipoamua kujiunga na chuo cha Ustawi wa jamii alafu masomo taiti mkwanja ishu kupatikana.
Ray na Mchomvu |
Clouds
Aliingia clouds mwaka 2010 mwishoni alipoitwa kuziba pengo la mtangazaji mmoja mahiri na mkongwe hata hivyo hakuweza ku cover ile chans ikabidi awe anaingia kwenye Segment fupi fupi mpaka alipo kabidhiwa kipindi cha Top 20 ndipo alipoona maisha mazuri mpaka sasa anaskuma GX100 na kununua kiwanja Bunju.
Maisha ya street
Ray alikuwa bonge la mdananda sana ila kutokana na muonekano wake kuwa kama Mhe.Joseph Mbilinyi(SUGU) basi ukimuona utajua sugu ukimuuliza anamaliza kuwa sugu bro wake,jamaa ana marafiki wengi saana kila kona hii ni kutokana na kuwa na upendo sana na kila mtu ana show luv,then jamaa anapenda sana kuvaa ku look gud,pia Ray ni mcheshi sana sijui hii inatokana na ile dhana ya vibonge wacheshi sana.
Malengo ya Ray
Kwasasa ana tumia muda wake mwingi sana kuandaa kipindi chake ambayo ndo na Career yake kinachoruka kila Jumapili saa5 asubuhi hadi saa7 mchana,pia ana malengo ya kumiliki kampuni yake binafsi au kiwanda na hii kutokana na kuwa na bachelar ya mambo ya viwanda,pia hana mpango wa kuoa kwasasa lakini hapo baadae mungu akimjaalia mke mwema.
Tribe:Mpare
Birth:29 july 1987
Home:Mbezi beach
Maritual:Single
Education:Industrial Relation(Bachelar)
Work:Creative designer at Clouds media
No comments:
Post a Comment